Mahakama nchini Korea Kusini imeunga mkono uamuzi wa bunge wa kumuondoa rais wa taifa hilo Park Geun-hye madarakani.

Mahakama hiyo ya kikatiba imesema kuwa bi Park alikiuka sheria na kuharibu demokrasia.

Park ambaye ndio mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini humo alihusishwa na kashfa ya kujipatia fedha kwa njia za ufisadi kutoka makampuni makubwa nchini humo na rafikiye mkubwa Choi Soon-Sil.

Bi Park huenda akakabiliwa na mashataka ya uhalifu.

Uamuzi huo ulipokelewa kwa shangwe katika maeneo mbali mbali yalio na wapinzani wa rais huyo.

Lakini wafuasi wake pia walionekana na kumekuwa na mzozano kati ya makundi hayo mawili.

Rais huyo sasa amepokonywa uwezo wa kutoshtakiwa na sasa anaweza kusimamishwa kizimbani na kufunguliwa mashtaka.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *