Mahakama ya Rufaa nchini Marekani imetupilia mbali rufaa ya marufuku iliyowekwa na Rais Donald Trump ya wasafiri kutoka nchi saba za kiislamu na Wakimbizi wote kuingia nchini humo.
Jopo la Majaji watatu kwa kauli moja limekataa kuupindua uamuzi uliotolewa na Jaji kutoka mji wa Seattle, ambaye wiki iliyopita alizizuia sehemu za amri iliyotolewa na Rais huyo wa Marekani.
Na muda mfupi tu baada ya Uamuzi huo wa mahakama kutangazwa, Trump aliwaambia waandishi wa habari kwamba ana uhakika mwisho wake ataibuka mshindi.
Katika hatua nyingine tena Rais Trump ametangaza mfululizo wa amri za Rais kwa lengo la kupunguza uhalifu. Akizungumza wakati wav kuapishwa kwa Mwanasheria mkuu wa nchi hiyo, Rais wa Marekani amesema uhalifu umeongezeka nchini Marekani na utawala wake utalishughulikia suala hilo kuamzia sasa.
Amri hizo zilizotangazwa ni pamoja na kukabiliana na magenge ya madawa ya kulevya na wafanyabiashara za kihalifu.