Mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini imeamuru kuwa kura ya kutokuwa na imani na Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma inaweza kufanywa kwa siri.
Mahakama ya katiba imesema kuwa spika wa bunge na haki ya kuamuru hatua kama hiyo. Awali alisema kuwa hakuwa na mamlaka kama hiyo.
Vyama vya upnzani vinaamini kuwa chini ya kura ya siri, wabunge kutokla chama cha Zuma cha ANC wanaweza kupiga kura ya kumpinga.
Bwana Zuma amekuwa chini ya shinikizo kufuatia shutuma nyingi ikiwemo madai ya ufisadi na mabadiliko kwa baraza la mawaziri yaliyokumbwa na utata.
Akitoa uamuzi huo Jaji mkuu Mgoeng Mgoeng, alisema kuwa spika wa bunge ana mamlaka ya kuamua ni njia gan kura hiyo itafanyika.
Spika wa bunge Baleka Mbete ni afisa wa cheo cha wa ANC na alikuwa amedai kuwa sheria za bunge haziruhusu kufanyika kura ya siri,