Mahakama nchini Afrika Kusini imekataa ombi la nchini hiyo kujiondoa Mahakama ya Kimataifa ya makosa ya uhalifu wa kivita (ICC) kwa madai kwamba uamuzi huo ni kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Afrika Kusini iliarifu Umoja wa Mataifa kuhusu lengo lake la kutaka kujiondoa ikiishtumu mahakama hiyo kwa kukandamiza uhuru wake.

Lakini chama cha upinzani cha Democratic Alliance DA kilisema kuwa serikali lazima itafute uungwaji mkono bungeni kuhusu suala hilo.

Mahakama hiyo iliagiza serikali kufutilia mbali notisi yake ya kutaka kujiondoa katika mahakama hiyo.

Uamuzi wa kutakankujiondoa ulijiri kufuatia mgogoro kuhusu ziara ya rais wa Sudan Omar al Bashir nchini humo mwaka 2015.

Mamlaka ya Afrika Kusini ilikataa kumkamata Bashir licha ya kuwa amewekewa agizo la kukamatwa na mahakama hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *