Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), imetoa huku ya kwanza juu ya pingamizi la nchi ya Kenya na kudai ina haki ya kuamua juu ya mgogoro wa mpaka baina ya nchi hiyo na Somalia.

Mgogoro huo ulianza baada ya Somalia kuomba mpaka wake wa bahari kuongezwa upande wa kusini na hivyo kupeleka kesi hiyo mahakamani.

Baada ya Somalia kupeleka malalamiko yake kwenye mahakama hiyo, Kenya ilitoa hoja ya kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Hata hivyo mahakama hiyo iliyopo The Hague, imetupilia mbali hoja hiyo ya Kenya.

Somalia na Kenya zimekuwa kwenye mgogoro kwa muda mrefu kuhusiana na kipande cha sehemu ya bahari ya Hindi ambacho kinadaiwa kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta na gesi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kesi hiyo inaweza kuchukua miaka kadhaa kuweza kufahamu iwapo mpaka wa bahari za Somalia utaongezwa au la.

kenya-somali-border

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *