Mahakama Kuu ya Tanzania imeamuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini  Sheikh Issa Ponda dhidi ya rufaa ilityokatwa na Jamhuri kupinga hukumu ya Mahakama ya Morogoro kumuachia huru kiongozi huyo.

Sheikh Ponda ameachiwa huru leo mbele ya Jaji Johnson Mkasimongwa ambaye amesema anakubaliana na uamuzi wa Mahakama ya Morogoro kumuachia huru Sheikh Ponda katika kesi ya kutoa matamshi ya uchochezi.

Aidha Jaji Mkasimongwa amefafanua  kwamba upande Jamhri haikupaswa kumshtaki Sheikh Ponda kwa kosa lile la kuvunja amri ya Mahakama ya Kisutu bali ilitakiwa wamrudishe katika Mahakama hiyo ili imchukulie hatua zaidi.

August 10, 2013, katika eneo la Uwanja wa Ndege inadaiwa kwamba Ponda alitoa kauli za kichochezi kwa waumini wa kiislam ambapo mojawapo ya kauli ni ile aliyosema kwamba (Waislam) wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *