Mahakama ya Juu Kenya yashindwa kusikiliza kesi ya kuahirishwa kwa uchaguzi kutokana na ukosefu wa majaji wa kutosha mahakamani.

Jaji Mkuu David Maraga amesema baadhi ya majaji wamo nje ya nchi na wengine hawangeweza kufika mahakamani kwa sababu mbalimbali.

Kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa na wapiga kura watatu wakisema Tume ya Uchaguzi haiko tayari kuandaa uchaguzi huru na wa haki kesho.

Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu hakuweza kufika kortini baada ya kupigwa risasi kwa dereva wake jana jioni.

Jaji Ibrahim, ambaye amekuwa akiugua, yuko nje ya nchi.

Majaji Smokin Wanjala na jacktone Ojwang hawakuweza kufika kortini pia.

Jaji Njoki Ndung’u alikuwa amesafiri nje ya jiji la Nairobi na hakuweza kupata usafiri wa kumuwezesha kufika mahakamani kwa wakati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *