Mahakama kuu nchini Kenya leo imeanza kusikiliza kesi iwapo ushindi wa rais Uhuru Kenyatta ni halali au batili.

Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Kenya na tume ya Uchaguzi IEBC, baada ya uchaguzi wa marudio ya Oktoba 26.

Kesi tatu zimewasilishwa mbele ya majaji 6 wanaoongozwa na jaji mkuu David Maraga, mbili zikitaka ushindi wa rais Kenyatta ubatilishwe, huku moja ikitaka viongozi wa upinzani wakiongozwa na Raila Odinga wachukuliwe hatua kwa madai ya kuchochea wafuasi wao kususia uchaguzi, na kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi.

Kesi za kubatilisha ushindi wa rais Kenyatta zimewasilishwa kwa misingi kwamba tume ya uchaguzi ilikosa kuagiza uteuzi mpya wa chama ufanyike baada ya mahakama ya upeo wa juu zaidi kufutilia mbali ushindi wa rais Kenyatta mwezi Agosti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *