Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemtaka Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kurekebisha hati ya mashtaka na kumwingiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, katika kesi yake ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa kanda hiyo, Camilius Wambura.
Pia mahakama hiyo imetoa zuio la muda kwa Jeshi la Polisi kuacha kumkamata Mwenyekiti huyo hadi maombi yake ya kupinga kukamatwa aliyowasilisha mahakamani hapjana yatakaposikilizwa Ijumaa Februari 24, mwaka huu, saa saba mchana.
Mbowe ametakiwa kuwasilisha hati yake ya mashtaka baada ya kuifanyia marekesho siku ya Jumatatu, Februari 26, mwaka huu.
Kamanda Wambura pekee kati ya walalamikiwa waliotajwa katika kesi hiyo ndiye aliyeonekana mahakamani hapo lakini Kamanda Sirro na Paul Makonda hawakutokea mahakamani hapo.
Mbowe anasimamiwa na mawakili Peter Kibatala, Tundu Lissu, Albert Msando, na John Mallya
Kesi hiyo itasikilizwa tena Machi, 8 mwaka huu baada ya kuhairishwa leo katika mahakama kuu leo.