Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli leo ataongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakachofanyika jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho ni cha kwanza kuongozwa na Rais John Magufuli tangu achaguliwe kukiongoza chama hicho tawala Julai mwaka huu.

Juzi, Rais Magufuli aliongoza kikao cha Kamati Kuu ambacho kilipaswa kuwa cha siku mbili, lakini kikamaliza kazi zake juzi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye aliwaambia waandishi wa habari juzi baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu kwamba mapendekezo au hoja zote zilizoibuliwa na wajumbe katika kikao hicho zitawasilishwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ambacho kitafanyika jijini Dar es Salaam.

Nape hakueleza hoja na mapendekezo hayo yanayopelekwa NEC, lakini kwa ujumla kikao hicho ndicho chenye uamuzi wa kubariki mapendekezo yanayotoka katika kikao cha Kamati Kuu hivyo inatarajiwa kuwa itafanya maamuzi mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *