Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamisha Mohammed Mpinga amesema kikosi hicho kitaanza kukamata magari yote ambayo yamewekwa taa zenye mwanga mkali (spotlights).

Mpinga amesema wameshatoa maelekezo kwa askari wa usalama barabarani, kuhakikisha wanakamata magari, pikipiki na malori makubwa ambayo yamewekwa taa hizo.

Kamanda Mpinga amesema kuwa walishatoa muda wa kutosha kwa wamiliki wote wa magari, walioweka taa hizo kuziondoa, hivyo kwa sasa wataanza kuwachukulia hatua wote ambao watakuwa hawajaziondoa.

Amefafanua kuwa uwekaji wa taa hizo ni kinyume cha Sheria ya Usalama Barabarani Kifungu cha 39 Sura ya 168, ambacho kinaeleza matumizi ya taa.

 Mpinga pia amesema magari yatakayokamatwa ni yale ambayo yameongezewa taa hizo ambazo ni kinyume na sheria ya usalama barabarani.

Amesema wamiliki wa magari hayo ya kuwindia, wanatakiwa kuondoa kava hizo wanapokuwa porini tu na kuongeza kuwa mtindo wa wamiliki wa magari makubwa kuweka taa nyuma ya magari ambayo inamulika, matokeo yake mtu anayemfuata anafikiri gari anakuja kumbe inakwenda mbele.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *