Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (Udart) umeamua kuhamisha ofisi zake kwa muda ili kuepusha uharibifu unaoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.

Ofisi hizo zilizopo eneo la Jangwani, wilaya ya Ilala, kwa sasa hazitatumika na mabasi yote yaendayo haraka yatalazwa katika vituo vikuu vya mabasi hayo.

Akizungumza leo Machi 16 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Udart,  Deus Bugaywa amesema wamehamisha ofisi hizo ili shughuli zinazofanywa na mradi huo zisiweze kutetereka kutokana na mvua zinazoendelea.

“Maji yalianza kujaa saa nane usiku, tulianza kuhamisha magari yetu yote na kuyapeleka katika vituo vikubwa vya mabasi yetu, licha ya mabasi pia tumehamisha vitu vingi vya ofisi kwa sasa hatutaitumia kwa muda,” amesema Bugaywa.

Amesema wameamua kusitisha huduma za usafiri wa mwendokasi leo, kutokana na maji kujaa eneo la jangwani na hivyo barabara hiyo ilifungwua tangu saa kumi alfajiri na imefunguliwa saa tatu asubuhi baada ya trafiki kujiridhisha kwamba inafaa kupitika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *