Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu ameonekana kufanya vizuri katika anga ya muziki wa Bongo Fleva toka ajiunge na lebo ya WCB.

Mrembo huyo amefanya makubwa chini ya Lebo ya WCB ambapo inasemekana kwa sasa ana jeuri mbele ya bosi wake, Diamond Platnumz kwa sababu mauzo yake yanatisha.

Tayari Zuchu amefikisha streams (watazamaji/ wasikilizaji) zaidi ya milioni 70 katika Mtandao wa Boomplay akiongoza Afrika Mashariki upande wa wasanii wa kike.

Mwaka 2020 alifikisha streams milioni 12 na kumfanya kuwa msanii wa kike aliyesikilizwa zaidi kwenye mtandaoni huo kwa mwaka huo.

Mwaka 2021 alifikisha streams milioni 37 na kuandika rekodi kama msanii wa kike duniani aliyesikilizwa zaidi kwenye mtandaoni huo.

Mwaka 2022 hadi sasa ametoa wimbo mmoja tu wa Mwambieni, lakini tayari amejikusanyia streams zaidi ya milioni 24 hivyo anaongoza Afrika Mashariki upande wa wasanii wa kike.

Kwenye mtandao huo, Zuchu ana nyimbo nne zenye streams zaidi ya milioni 10 sawa na Diamond Platnumz au Mondi akifuatiwa na Jovial wa Kenya mwenye nyimbo tatu kisha Rayvanyy na Otile Brown (Kenya) ambao wote wana mbili.

Kwa jumla, kwa ujumla wasanii wenye streams nyingi Boomplay Afrika Mashariki ni Diamond, Rayvanny, Mbosso na Zuchu; wote kutoka WCB.

Ikumbukwe Extended Playlist (EP) ya Zuchu ya I Am Zuchu yenye nyimbo saba ilikaa tano bora kwenye chati za Boomplay kwa wiki 75 huku ukishika namba moja kwa wiki 35.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *