Mwezi mmoja na wiki kadhaa zimepita toka uongozi wa lebo ya Next Level Music inayomilikiwa na Rayvanny imtangaze Mac Voice kama msanii wakwanza chini ya lebo hiyo msanii huyo amepata mafanikio haya makubwa ndani ya kipindi hicho kifupi.
Mafaniko hayo ni pamoja na kutajwa kwenye tuzo za AEAUSA kwenye kipengele cha Best New Artist, kuvuna zaidi ya streams Milioni 4 kwenye mtandao wa Boomplay hukua akiwa na subscribers karibia lakini moja (100,000) kwenye mtandao wa YouTube.
Si hivyo tu Macvoice amevuna watazamaji zaidi ya Milioni 4 kwenye mtandao wa YouTube, kualikwa kwenye shows na mwisho kabisa kuingia kwenye orodha ya wasanii 10 waliotazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube mwezi October 2021.
Kupitia ukurasa wa instagram wa CEO wa lebo hiyo ameandika ujumbe huu kumpongeza msanii wake huyo Rayvanny ameandika “Nilikwambia Usiwaze kushindana mdogo wangu Mac Voice. Unaona jinsi Mungu anavyokunyenyua keep making us proud Mac Voice.