Klabu ya Real Madrid imerejesha mipango yake ya kumuwania kipa David De Gea kutoka Manchester United kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amefikia uamuzi huo bada ya kukosa matumaini ya kumsajili Kylian Mbappe kutoka Monaco.
De Gea ilibaki kidogo ajiunge na Madrid mwaka 2015 kabla ya kushindikana dakika za mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili msimu huo.
Kutokana na tetesi hzio Manchester United haijatoa kauli ya mwisho kuhusu harakati hizo za Madrid kwa De Gea huku yenyewe ikiwa inamuwania Thomas Lemar kutoka Monaco na imeweka dau la pauni milioni 55 mezani.
Madrid wanataka kumsajili kipa huyo kutokana na kutokuwa na imani na kipa wao Narvas licha ya kuwasaidia kutwa makombe tofauti msimu uliopita.