Madereva wa daladala katika kituo cha Simu 2,000 jijini Dar es Salaam wamegoma kutoa huduma ya usafiri kuanzia leo Jumatatu wakipinga ongezeko la ushuru kituoni hapo kutoka Sh 500 hadi Sh 1,000.

Madereva hao wamelalamikia kitendo cha Manispaa ya Ubungo kuwapandishia gharama za ushuru wakati hali ya uchumi na biashara kwa ujumla ni ngumu kwao kwasasa.

Mmoja wa madereva katika kituo hiko amesema kuwa takribani mwezi mmoja uliopita katibu wa soko aliwaletea notisi ya mwezi mmoja ikieleza kuwa ushuru utapanda kutoka Sh 500 hadi Sh 1,000 lakini wao walikataa.

Pia amesema kuwa walipeleka malalamiko yao kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda lakini wakashangaa kabla ya maamuzi ya mkuu mkoa jana walipewa vipeperushi vilivyoeleza kuanzia leo ushuru unapanda kutoka shilingi 5,00 hadi kufikia 1,000.

Kwa upande wao abiria wamelalamikia kitendo cha kukosa ufasiri kituoni hapo tangu alfajiri jambo ambalo limewafanya kuchelewa kufika kwenye maeneo yao ya kazi kutokana na usumbufu uliojitokeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *