Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Madee amesema kuwa iwapo mwanae wa kike, Aimal Hamad  atachagua kuwa msanii kama yeye atamruhusu bila wasiwasi.

Madee amesema kuwa atamhuruhusu mwanae huyo kufanya muziki kwasababu hata yeye pia amefuata nyayo za baba yake katika fani hiyo.

Madee amesema kuwa licha ya mwanae hata studio hajui ilipo lakini iwapo atapenda muziki yeye kama mzazi hawezi kumuwekea mipaka mtoto wake huyo.

Madee ameongeza kwa kusema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi kwenye Sanaa kwa wanawake lakini hana budi kumruhusu mwanae huyo kuonyesha kipaji chake kwa kuwa kila mtu amepangiwa ridhiki yake.

Msanii huyo amesema kuwa wazazi wanashauriwa kuwaangalia watoto wao wafanye kitu wanachotaka hivyo hawezi kumpangia mtoto wake kitu cha kufanya katika maisha yake.

Madee amesisitiza na kuwataka wazazi kuwaachia watoto kufanya wanachotaka na si kuwachagulia katika maisha yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *