Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutokea pande za Tip Top Connection, Madee amefunguka na kusema kuwa avutiwi na uvaaji wa msanii mwenzake Roma Mkatoliki.
Madee amesema kuwa Roma anavaa kawaida sana kama vile siyo msanii jambo ambalo alitaka kumrekebisha hapo awali kutokana na mtindo wake wa mavazi.
Msanii huyo ameendelea na kusema kuwa katika wasanii wote wa Bongo ni Roma peke yake ndiyo anamuangusha kwenye suala la mavazi mpaka anatamani siku ampeleke dukani akamchagulie nguo.
Kauli ya Madee inaweza kuchukuliwa ni kawaida kwa wasanii waliochini ya Tip Top Connection kwani kipindi cha nyuma Dogo Janja aliwahi kutoa kauli inayoshabiana na hiyo kwa kueleza hakuna msanii Bongo anayemfikia kwa kuvaa vizuri.
Kwa upande wa Roma bado hakujibu kauli hiyo ya Madee kuhusu uvaaji wake ambapo amedai kuwa aendani na mavazi yake.