Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Madee amemtaka msanii wake Dogo Janja kupunguza safari ni muda wa kuachia wimbo mpya.
Madee ameweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter, lakini pia kupitia Instagram amefunguka kuwa kesho July 30,2022 ataachia wimbo mpya kutoka kwa Dogo Janja.
Madee amempa ushauri mwanamuziki huyo baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kuachia ngoma yoyote kwa muda mrefu.
Dogo Janja ni msanii ambaye ana milikiwa na Madee kama boss wake kwenye ngazi ya muziki wa Bongo Fleva toka alipoanza kumsimamia mwanamuziki huyo.