Kaimu Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Global Resource Alliance, Madaraka Nyerere ameiomba serikali kupunguza kodi katika bidhaa zinazotengeneza nishati ya jua.
Madaraka Nyerer ambaye ni mtoto mkubwa wa Mwl. Nyerere amesema hatua hiyo itawawezesha wananchi vijijini kupata nishati hiyo na hivyo kupungu za matumizi ya kuni na mkaa inayochangia kuharibu misitu.
Madaraka amesema shirika lake kwa kushirikiana na Kampuni ya GoSol Ltd kutoka Finland limebuni jiko la kutumia mionzi ya jua.
Amesema jiko hilo litakuwa ukombozi kwa wajasiriamali wadogo vijijini ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za umeme, mafuta na gesi.
Kwa uapnde wake Meneja Mradi wa GoSol kutoka Finland, Heikki Lindfors amssema jiko hilo ni ukombozi kwa wakazi wa vijijini zaidi ya bilioni tatu duniani.
Pia amesema jiko hilo linaweza kuokoa zaidi ya tani tisa ya miti inayokatwa kwa mwaka duniani.