Madaktari nchini Kenya wamekataa nyongeza iliyopendekezwa na serikali katika juhudi za kujaribu kumaliza mgomo wa madaktari na wahudumu wa afya ambao umedumu kwa mwezi mmoja sasa.

Rais Uhuru Kenyatta alikutana na wawakilishi wa chama cha taifa cha madaktari hao Jumanne na kupendekeza nyongeza ya mshahara na marupurupu ya madaktarii kwa angalau $560 (£450).

Viongozi wa chama hicho, ambao walikuwa wameahidi kutangaza msimamo leo, walisema pendekezo la serikali linawafaa madaktari lakini kuna baadhi ya mambo ya kuwafaa wananchi ambayo yameachwa nje.

Madaktari wanaitaka serikali kutekeleza makubaliano ya mishahara na marupurupu yaliyotiwa saini mwaka 2013.

Kwenye makubaliano hayo, serikali iliahidi kuongeza idadi ya madaktari, kuongeza pesa za utafiti wa kimatibabu, dawa na vifaa na mitambo katika hospitali za umma.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *