Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF), Jenerali Venance Mabeyo amefunguka na kuweka wazi kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameweka historia katika jeshi hilo toka kuanzishwa kwake kwa Mkuu wa Majeshi kuwavisha vyeo maafisa wakuu akiwa Ikulu.
Jenerali Venance Mabeyo amesema hayo leo wakati Rais Magufuli akimuapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luten Jenerali Yakubu Hassan Mohamed Ikulu Dar es Salaam na kusema yeye amekuwa Mkuu wa Majeshi wa kwanza kufanya zoezi hilo akiwa Ikulu na kusema yeye mwenyewe lilimpa hofu kidogo.
Aidha Mabeyo alimshukuru Rais Magufuli kwa kuweza kuwapandisha vyeo kuanzia Mnadhimu Mkuu, Luten Jenerali Yakubu Hassan Mohame na Majenerali Jacob Gidion Kingu, Martin.S.Busungu, Alfred Fabian Kapinga, Kesi Philip Njelekela
Wengine Rais aliowapandisha vyeo ni, Anselmo Shigongo Bahati, Methiew Edward Mkingule, Blasius Kalima Masanja, Ramadhani.R.Mrangira, Shija Seifu Makona na George Thomas Msongole.