Mahakama kuu nchini Zimbabwe imetoa ruhusa kwa wafuasi wa vyama vya upinzani kuandamana kwenye mji mkuu wan chi hiyo Harare kuanzia saa sita mchana hadi saa kumi alasiri.
Hata hivyo amri hiyo ya mahakama kwa siku ya jana ilitanguliwa na vurugu za kutupiana mawe na mabomu ya machozi baina ya polisi na wananchi.
Maandamaon hayo yaliyoratibiwa na muungano wa vyama vya upinzani nchini humo unaoitwa National Electoral Reform Agenda (Nera) yanataka kubadilishwa kwa mfumo wa chaguzi za viongozi wa kisiasa nchini humo.
Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC), Douglas Mwonzora alisema kuwa waandamanaji wamejizatiti na wamedhamiria kupata wanachokidai.
‘Licha ya mabomu ya machozi kwenye eneo letu la mkutano kutaendelea na maandamano. Sio harusi. Tunajua hilo. Haitokuwa rahisi. Tutaenda kuandamana bila kujali iwapo watatupiga au la’.