Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inatarajia kutoa maamuzi baada ya kupitia mahojiano kati ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na kituo cha radio cha Times Fm.
Kamati ya maudhui ya TCRA iliyokuwa ikifanya uchunguzi huo inakaribia kumaliza kazi hiyo ndani ya wiki hii
Machi 22, 2018, Times ilipokea barua ya kuwataka wawasilishe kipindi hicho kilichorushwa Machi 19, 2018 na kutii agizo hilo.
Mwanamuzi Diamond alizua mjadala baada ya kuzungumzia suala la nyimbo za wasanii hao kufungiwa akimlalamikia Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kutowatendea haki wasanii.
Ofisa Mkuu Idara ya Utangazaji wa mamlaka hiyo, Andrew Kisaka amesema kwamba tayari kamati ya maudhui inakaribia kumaliza kazi yake ya kupitia maudhui ya kipindi hicho.