Maafisa watatu wakuu wa jeshi ndani ya serikali ya Sudan Kusini wamejiuzulu nchini humo kutokana na uhalifu unaofanywa na serikali hiyo.

Makamanda hao wamejiondoa serikalini wakimlaumu Rais Salva Kiir kwa kuhusika katika uhalifu wa kivita na mauwaji yanayolenga kabila fulani.

Brigedia Henry Oyay Nyago, anamshutumu Rais ambaye anatoka katika kabila la Dinka, kwa kuamuru kuwauwa kwa watu wasiotoka katika kabila hilo la Dinka.

Kanali Khalid Ono Loki, pia anamlaumu kiongozi mkuu wa jeshi kwa mauwaji ya kimbari, kukamatwa na kuwazuilia watu kiholela.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *