Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva anatarajia kuungana na Hamisa Mobetto katika uzinduzi wa Lipstick zake nchini Uingereza.

Hamisa Mobetto anatarajia kuzindua rasmi lipstick zake zinazojulikana Kama “Charmed Cosmetic” nchini Uingereza ifikapo mwezi wa tano.

Kwenye uzinduzi huo utakaofanyika tarehe 5 Mei 2018, utasindikizwa na burudani toka kwa Lulu Diva ambaye ametoa wimbo wake mpya hivi karibuni unaoenda kwa jina la Huba.

Hamisa alitangaza habari hiyo njema kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *