Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Lulu Diva afunguka na kusema kuwa anatarajia kufanya kolabo na Wizkid.
Lulu Diva amesema kuwa mwakani kuna uwezekano wa kufanyika kolabo hiyo kwani mipango yote imeshapangwa bado utekezaji wa kolabo hiyo.
Amesema kuwa “Watengemee kolabo may be Wizkid, alikuwa rafiki yangu lakini tulikuwa tunachati na kukutana naye nafikri nakumbuka ile party Diamond alifanya Mwanza Wizkid alikuja ku-perform hapo ndio nilionana naye kwa mara kwanza”.
Pia amesema kwa upande wa wasanii wa Bongo wapo wasanii wengi ambao anawafikiria lakini kwa sasa anatamani kuja kufanya kolabo na Vanessa Mdee alafu baadae ndiyo ataamua kufanya na wengine.
Mwanamuziki huyo anayetamba na wimbo wake ‘Give It To Me’ amesema kuwa kama ngoma yake na Wizkid itakamilika basi itamtambulisha vizuri katika ramani ya muziki barani Afrika na Ulaya kutoakana na umahiri na umaarufu alionao Wizkid.