Wasanii wa Bongo Fleva, Lulu Diva, Amber Lulu na Gigy Money wametangazwa rasmi kuwa watakutana kwenye jukwaa moja la Burudani jijini Mwanza.

Wasanii hao wenye rekodi nzuri ya kuteka chati za muziki na mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi wametangazwa kukutanishwa na ‘SISTAZ CONCERT’, tamasha itakalofanyika Juni 25 2022, Club Elevate, Malaika Beach jijini humo.

Tamasha hilo lililoandaliwa na Fresh by cooge litaongozwa na Ammy Gal, jukumu la burudani ya muziki akikabidhiwa kwa dj mamaie huku watakaohudhuria wakitarajia pia kumshuhudia mwigizaji Wema Sepetu.

Wasanii hao wamewataka mashabiki wao wajitokeze kwa wengi kwenye tamasha hilo litakalofanyika jijini Mwanza hivyo wamewataka mashabiki wao kujitokeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *