Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amefunguka na kusema kuwa hataki kufananishwa na msanii mwenzake Shilole.
Kauli hiyo imekuja baada ya kuenea kwa taarifa za wawili hao kushindana kutokana na aina ya muziki wao wanaofanya.
Lulu Diva amewataka mashabiki ambao wanafananisha rekodi zake na na miondoko ya nyimbo za Shilole waache kumpambanisha naye kwani hataki beef naye.
Mwanamuziki huyo amedai kuwa anamheshimu Shilole kama dada yake hivyo hatopenda kuingia kwenye mgogoro na Shilole.
Amesema kuwa Hapana Jamani hakuna mtu ambaye anapotezwa kila mmoja anaimba mziki wake na mimi Shilole namheshimu kama dada na anafanya mziki wake wa kwake peke yake yaani hata ukiangalia mziki anaofanya na mziki wangu ni vitu viwili tofauti ni watu tu wanatengeneza vitu ili waweze kutuchonganisha”.