Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amefunguka na kukanusha habari kuwa amepokonywa kila kitu na aliyekuwa mpenzi wake baada ya kagombana.

Kauli hiyo ya Lulu Diva inakuja kufuatia tetesi zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa mwanadada huyo amepokonywa kila kitu na mwanaume wake baada ya kuachana jambo ambalo Lulu Diva amelipinga vikali.

Lulu Diva amesema kuwa ni kweli amegombana na mwanaume wake huyo na hayupo nae tena kwenye mahusiano ila hawezi kumyanga’nya vitu kwani vitu vingi ni vya kwake hivyo hawezi fanya hivyo.

Siku chache zilizopita mwanamuziki huyo aliviteka vichwa vya habari kuwa chanzo cha kugombana na mwanaume wake huyo ni baada ya kuanzisha mahusiano na mwanamuziki kutoka WCB, Rich Mavoko.

Pia Lulu Diva amesema kuwa hana mahusiano na Rich Mavoko kwani ni rafiki yake wa karibu sana ila hana mahusiano naye.

Mwanadada huyo kwasasa anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Amezoea’ ambao unafanya vizuri katika media mbali mbali nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *