Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva ameamua kufunguka kwa mara ya kwanza kuhusu video zake za utupu kusambaa mitandaoni na kuibua sintofahamu miongoni mwa mashabiki zake na watu wake wa karibu.

Lulu amesema Video hizo zimesambazwa na aliyekuwa mpenzi wake akidai kuwa anataka kumkomesha mrembo huyo na kumharibia maisha yake.

“Alikuwa anafosi anamwambia…. kwa nini hauposti, mbona huweki vitu? I want Lulu to die, afe kabisa asiishi katika haya maisha. Sijui hata nilichomfanyia ni nini, kuachana kila mtu anaachana.

“Hakuna kitu kikubwa alichoknifanyia kwenye maisha yangu mpaka afikie hatua ya kusema anataka kuniharibia maisha, meseji hizo hapo mnaziona ambazo alikuwa ananiambia.

“Kama ninavyokwambia, nilikuwa naongea naye kimapenzi kama mpenzi wangu, ni mtu ambaye najiamini kuongea naye kwa sababu alinipenda, namuona ni mtu mzima, ana umri wa miaka 55, ametulia, kwa hiyo huwezi kufikiria kama anaweza kufanya vitu kama hivyo na mimi nilikuwa tayari kutulia.

“Kwa sasa hivi mimi nimetulia najiuguza, naangalia tu afya yangu, lakini pia kumuomba Mungu, ni jambo jema kumuomba Mungu kwa sababu najua nimemkosea kutokana na kitu nilichokifanya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *