Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amefunguka na kusema kuwa anatarajia kumshirikisha mwanamuziki wa Marekani Card B kwenye nyimbo itakayokuwa kwenye albam yake mpya.
Lulu Diva amesema kuwa kutoka na muziki kurudi kwenye mfumo wa albam kama zamani hivyo mbioni kuja na albam yake mpya ambayo itakuwa ya kwanza kuiachia toka aanze shughuli za kuimba.
Pia Lulu Diva alisema muziki umehamia kwenye albamu na ni heshima pia kufanya kazi nzuri ambayo hata baadaye inabaki kwenye historia hivyo kumshirikisha Cardi B ni chachu ya kutangaza muziki wake kimataifa zaidi.
“Najiandaa kufanya albamu kama ambavyo wanamuziki wakubwa wamekuwa wakifanya hivi karibuni na albamu yangu itakuwa imesheheni wanamuziki wakali ndani na nje ya Afrika na ndani yake nitamshirikisha Cardi B, kutoka Marekani, nafurahi sana maana naona nikitoka kimataifa zaidi kwa kweli,”.
Soko la albam kwasasa limerudi kwa kasi baada ya wasanii kadhaa kuachia albam zao mpya na kufanya vizuri sokoni kama vile, Vanesa Mdee, Diamond Platnumz na Lady Jay Dee.