Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva ambaye anadaiwa kulazwa hospitalini kwa mshtuko baada ya video yake chafu kuvuja na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Video hiyo chafu ya Lulu Diva imewaibua watu wengi ambao wanasema kuwa ishu hiyo iwe funzo kwa kina dada ambao wamekuwa vichwa ngumu kujifunza kwa wenzeo.
Imeelezwa kuwa, mara zote ambazo video hizo zimesambaa, basi asilimia 90 ya video hizo anayeonekana kuathirika, kushambuliwa mwanamke.
Pia imeelezwa kuwa, koneksheni ya mwanaume inakuwa kama siyo ishu kubwa na watu hawajali kivile, lakini zinapovuja za kina dada inakuwa ni ishu kubwa.
Wataalam wanasema kuwa, mtu anayetaka umtumie picha au videos zako za utupu ni kuwa hana malengo na wewe na wala hakuheshimu ila anayekuheshimu siyo rahisi kukurekodi au kukuambia jirekodi umtumie hivyo cha muhimu ni kumkimbia au kumkataa mtu au mpenzi anayehitaji mambo kama hayo.