Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kuzaa mtoto kwa hivi sasa labda baada ya miaka mitano.
Lulu Diva amesema kuwa kwasasa hawezi kuzaa kwasababu bado hajatimiza malengo yake katika maisha na kazi yake ya muziki hivyo kuzaa hatasubiri sana.
Kauli ya mwanadada huyo inakuja baada ya video queen Bongo, Gigy Money kujifungua mtoto wa kike aliyezaa na mtangazaji Mo Jay.
Lulu Diva ameweka wazi licha ya kuwa Diamond alimtaka azae mtoto hivi karibuni na yeye akakubali hjamaanisha atazaa siku za hivi karibuni kwani hana mpango wa kuzaa mpaka miaka mitano ipite.
Pia Lulu Diva aliendelea kukataa kuongelea Mahusiano Yake na Rich mavoko huku akidai hayo ni maisha yake binafsi.