Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amefunguka na kusema kuwa hana mpango wa kuolewa kwasasa.
Kauli hiyo ya Lulu Diva inakuja kufuatia mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole kufanya sherehe ya ndoa na mpenzi wake Uchebe wiki iliyopita.
Lulu Diva amesema kuwa hafikirii maisha ya ndoa wala kuwa na uhusiano na staa Bongo kwani atapata presha tu kwenye mahusiano hayo.
Amesema kuwa “Kama kuoana acha waoane wao lakini kwangu noo! Nimeingia kwenye muziki kwa hiyo focus yangu yote ipo hapo, sijawahi kufikiria hata kuwa na mpenzi msanii.
Hivi karibuni mastaa wa Bongo walifunga ndoa ambapo Dogo Janja alifunga ndoa na Irene Uwoya huku Shilole akiolewa na Uchebe.