Muigizaji wa Bongo Movie, Elizaberth Michael maarufu kama Lulu amefunguka na kusema kuwa hana tofauti na muigizaji mwenzake Wema Sepetu licha kutokuwa na mawasiliano.

Lulu amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Royal Tour uliofanyika mkoani Arusha ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliongoza uzinduzi huo.

Lulu amesema kuwa hana tofauti na muigizaji mwenzake huo ila walikuwa wanamikwaruzano ya kawaida lakini hana bifu kabisa na anamuheshimu kama dada yake.

Wawili hao walionekana katika sherehe ya mtoto wa muigizaji mwenzao, Irene Uwoya ambaye amepokea kipaimara yake.

Pia Lulu amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kusubili tamthilia yake ambapo ipo katika matayarisho ya kukamilika hivyo mashabiki wasubilie kwa hamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *