Muigizaji wa Bongo Movie, Elizaberth Michael (Lulu) amehukumiwa miaka miwili jela baada ya mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam kumkuta na hatia ya kuuwa bila kukusudia.

Mahakama kuu yamtia hatiani msanii huyo kwa kesi ya mauaji ya Steven Kanumba yaliyofanyika mwaka 2012.

Jaji aliyesimamia kesi hiyo, Sam Rumanyika amemtia hatiani huyo kwa kosa la kuua bila kukusudia na sasa amemtaka wakili wa upande wa utetezi, kama ana ombi lolote la kupunguziwa adhabu.

Jaji Sam Rumanyika amesema kifo kilitokana na ugomvi hivyo amejiridhisha kwamba mtuhumiwa aliua bila kukusudia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *