Muigizaji wa Bongo Movie, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amesema kuwa hivi sasa ni mtu wa kukaa nyumbani tu kila wakati kwa sababu ukweli ni kwamba hakuna starehe ambazo hajapitia au hakuna sehemu aliyoacha kwenda.

Lulu ambaye pia ni ni mfanyabiashara wa nguo mbalimbali za kike, amesema kuwa, anachoamini ni kwamba mambo ya zamani ilikuwa ni utoto tu na si kitu kingine.

Pia Lulu amesema kuwa hivi sasa amekuwa tofauti kabisa na ukichanganya na kulea, basi vitu vimebadilika kabisa na kikubwa zaidi kwake ni mtoto wake tu na si kitu kingine.

“Jamani naweza kusema maisha ya ujana yaacheni kabisa, yana mambo mengi sana, lakini Mungu ni mwema sana kwani kila kitu kimebadilika kabisa.

Pia amesema kuwa anaweza hata kumaliza miaka miwili bila kujua kabisa hata kumbi yoyote ya starehe, kwanza akili yangu iko kwa mtoto wangu ambaye ndiye amebadilisha kila kitu kwenye maisha yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *