Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi amepiga marufuku wananchi kuuza ardhi kwa wawekezaji wa kigeni bila ya ruhusa ya Serikali.

Waziri huyo ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilaya Magu mkoani Mwanza kwaajili ya kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 30.

Waziri Lukuvi amesema “Iko tabia na mazoea ya nchi hii,nyinyi wananchi wengi wa vijijini mmekuwa mnawaruhusu sana hawa wananchi wanaojiita wawekezaji, na wengi wao wanaokuja kununua ardhi kwa mtindo huu ni aina ya watu waliokuja kununua mwaka 84, hawa hawa watanzania wenye asili ya Asia mliowapa nyinyi, wananunua ardhi kwenu hawaendelezi, ardhi ile wanachukulia mapesa benki wanafika mahali halafu baadaye wanakuja kuuza,”.

Pia Lukuvi ameonya “Mtu yeyote leo ni marufuku kwa serikali ya wilaya kumkubalia au watu wangu wa wizara ya ardhi mtu yeyote hajaendeleza shamba ambaye hajaendeleza shamba amekaa nalo kwa miaka kumi hajaendeleza, halafu kwa ujanja ujanja anataka kuliuza kwa mtu mwingine au kulitumia kwa njia nyingine kutengeneza sijui viwanja na nini ni marufuku,”.

Kauli hiyo ya waziri Lukuvi inakuja kufuatia kushamili kwa vitendo vya uuzwaji holela wa ardhi kwa baadhi ya raia wa kigeni ambapo huwa wanafanya shughuli tofauti na matumizi ya ardhi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *