Mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku huenda hakakosa mechi tatu endapo atakutwa na kosa la kumpiga kwa kisigino wa beki wa Brighton, Gaetan Bong siku ya Jumamosi.

Kipande cha ‘video’ kimeonyesha Lukaku akimpiga kwa kisigino mara mbili beki huyo wakati wa kupigwa kwa mpira wa kona katika lango la Brighton dakika chache kabla ya kupatikana kwa bao lililowafanya United kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

FA tayari wanafahamu tukio hilo wanachosubiri ni ripoti ya muamuzi wa mchezo huo, Neil Swarbrick kabla ya kutoa maamuzi.

United imetumia kiasi cha paundi milioni 75 kumsajili Lukaku  ambaye bilashaka endapo maamuzi yatatolewa ataikosa michezo mitatu dhidi ya Watford, Arsenal na wamwisho ni Manchester derby katika dimba la Old Trafford Desemba 10.

Mwezi uliyopita beki wa Liverpool, Dejan Lovren alimlalamikia Lukaku kwa kitendo cha kumpiga teke la uso hali iliyopelekea kupatikana bao lililopelekea mchezo huo kutoka sare katika dimba la Anfield huku FA ikishindwa kuchukua hatua juu ya malalamiko hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *