Manchester United imeshinda 2-0 dhidi ya Manchester City katika mechi ya kirafiki iliyofanyika jana usiku nchini Marekani.

Romelu Lukaku na Marcus Rashford waliisaidia United katika mabao yote mawili yaliofungwa katika kipindi cha kwanza.

Kikosi hicho cha Jose Mourinho kilianza kwa mashambulizi huku Anders Herrera akianzisha juhudi hizo mapema, huku mashambulio mengine yakitoka nje ya eneo la hatari ,United wakimjaribu kipa mpya wa City Ederson.

David De Gea alilazimika kuwa macho katika upande mwengine huku Raheem Sterling akishambulia mara mbili , kabla ya Chris Smalling kuzuia mashambulizi mawili yaliofanywa na Patrick Roberts na Sterling.

United hatahivyo ilifanikiwa dakika nane kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza baada ya Lukaku kupata pasi muruwa kutoka kwa Paul Pogba na kucheka na wavu.

Dakika mbili baadaye Marcus Rashford aliifungia United bao la pili akifunga baada ya kazi nzuri kutoka kwa Henrikh Mkhitaryan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *