Wajumbe wa kamati kuu Chadema, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa, wameondoka katika mahakama ya Kisutu kabla viongozi wa CHADEMA hawajafikishwa mahakamni hapo.

Taarifa kutoka mahakama ya Kisutu zinasema kuwa kina Lowassa wameondoka eneo hilo huku wakitoa taarifa kuwa wanaelekea kwenye msiba wa mmoja wa wanachama wao.

Kwa mujibu wa mwanasheria wa kina Mbowe Peter Kibatala, amesema kuwa Mbowe na wenzake watano hawajafikishwa mahakamani hapo mpaka sasa, kusomewa shtaka linalowakabili.

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watano, hii leo wanatarajia kujua hatma ya dhamana yao juu ya kesi inayowakabili.

Source: East Televison

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *