Mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa ametuma salamu la rambirambi kufuatia kifo cha Waziri wa usalama wa Kenya, Meja mstaafu Joseph Nkaissery.

Meja Joseph Nkaissery alipelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya kabla ya umauti kumkuta.

Baada ya taarifa hizo kusambaa Waziri Mstaafu Edward Lowassa amesema Nkaissery alikuwa ni rafiki mzuri na kiongozi mzuri na wakupigiwa mfano

Lowassa amesema kuwa “Natuma salamu zangu za pole kwa familia na watu wa Kenya kwa kumpoteza Waziri Joseph Nkaissery, alikuwa ni rafiki mzuri na kiongozi mzuri wa kupigiwa mfano, Mungu amumlaze mahali pema peponi”.

Joseph Kasaine Ole Nkaissery alikuwa ni mwanasiasa wa Kenya, Mbunge kutoka mwaka 2002 mpaka 2014 na baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa usalama wa Kenya mpaka kifo chake, mbali na hilo Nkaissery alikuwa kiongozi Mkuu wa jamii ya Maasai nchini Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *