Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Edward Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa hatua anazozichukua kuhusu sakata la usafirishaji wa mchanga wa madini.

Lowassa  amesema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la mchanga wa madini (makinikia) ambalo limeonyesha kuwa Tanzania impoteza zaidi ya trilioni 100 tangu mwaka 1998 hadi Machi mwaka 2017.

Lowasa ambaye amesema kuwa anampongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza maamuzi ambayo ni ya UKAWA kwani kipindi anazunguka kuomba kura kwa wananchi alipopita maeneo yenye madini aliyazungumza haya yanayotekelezwa leo.

Pia amesema kuwa ni kweli mikataba ya madini ina matatizo na hata yeye alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu aliwaita wawekezaji hao wakakaa na kuzungumza, lakini jambo gumu lilikuwa ni kwamba, mikataba ukishaiweka saini inakuwa migumu sana kubadilisha.

Lowassa alieleza kwamba baada ya kuongea nao kwa muda walikubali na kuongeza kidogo mirahaba lakini haikutosha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *