Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema kwamba hana mpango kabisa na wala hafikirii kurudi CCM.
Lowassa ameyasema hayo kufuatia kauli iliyotolea na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho ambo, kwamba Lowassa ana mpango wa kurudi CCM kama baadhi ya wananchama wengine wa CHADEMA walivyofanya, na kusema kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote na haitakuja tokea.
Edward Lowassa ameendelea kwa kusema kwamba kitendo cha Mrisho Gambo ambaye ni mkuu wa mkoa wa Arusha kusema hadharani kwamba Lowassa amemuomba amkutanishe na Rais Magufuli kwani anataka kurudi kwenye chama, ni kitendo kisichofaa kwa kiongozi mkubwa kama yeye, na kumtaka aache mara moja kwani yeye sio msemaji wake.
Hivi karibuni Mrisho Gambo alisikika akisema kwamba amefuatwa na baadhi ya watu ambao wametumwa na Lowassa, kumuomba amsaidie kukutana na Rais Magufuli ili aweze kurejea CCM, kwani uamuzi ambao aliufanya mwaka 2015 wa kuhama chama ulikuwa ni uamuzi wa hasira.