Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa amefunguka kwa mara ya kwanza sababu ya kukutana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Lowassa ameamua kuweka wazi mambo ambayo amezungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kusema kuwa alikuwa akimshawishi kurudi CCM.
Lowassa ameweka wazi hilo leo Januari 15, 2017 na kusema kuwa Rais Magufuli alimuomba aende Ikulu ili waweze kukutana na kufanya mazungumzo.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje- CHADEMA, bwana John Mrema amethibitisha kuwa ujumbe huu ni kutoka kwa Edward Lowassa.