Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema kuwa ameohojiwa kwa saa nne katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi  wa Makosa ya Jinai (DCI).

Baada ya mahojiano hayo Lowassa ameachiwa kwa dhamana na kuondoka makao makuu ya polisi majira ya saa 8 mchana jana.

Lowassa amesema aliitwa kuhusu kauli aliyoitoa ya viongozi wa dini ya Kiislam wa Zanzibar (Uamsho) kuendelea kusota rumande kwa miaka kadhaa sasa kauli ambayo inadaiwa kuwa ni ya uchochezi.

Wakati wa futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) Lowassa alisema aliwaahidi wananchi endapo angechaguliwa kuwa rais angewatoa mashehe hao siku hiyo hiyo lakini anashangaa viongozi hao wa dini wanavyoendelea kusota rumande mpaka sasa bila kufahamu kosa lao.

Akizungumzia suala hilo, Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala amesema Lowassa amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena Alhamisi saa 6.00 mchana.

Kibatala amesema Lowassa amehojiwa kwa kosa la uchochezi na ameandika maelezo ya onyo juu ya kauli aliyoitoa wakati wa futari iliyoandaliwa na mbunge huyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *