Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Lord Eyes amefunguka na kusema kuwa hajawahi kumfundisha aliyekuwa mpenzi wake Ray C kutumia madawa ya kulevya bali alimkuta tayari kashatumia.
Kauli ya mwanamuziki huyo imekuja baada ya kuenea taarifa kuwa mwanamuziki huyo amemfundisha Ray C kutumia dawa za kulewa wakati wakiwa wapenzi.
Lord amesema kuwa “Nimekutana na Ray C tayari alikuwa ameshawahi kutumia japo mimi nilimficha, nikiwa naye situmii ila nikiwa na kampani yangu natumia, sasa hadi ile kampani yangu ikamfikia.
Pia ameendelea kusema sijawahi kumfundisha mtu, hata mimi nilikuwa sijui nilipewa nikaonja, Madawa ya kulevya ni kama shetani anavyokuingia, familia yangu ikawa inalia sana kama hujawahi kuonja usiguse hiyo kitu kiukweli”.
Aidha ameongeza kusema “Nilimpenda sana Ray C, hadi ilifika level ambayo nikawa namuogopa ila ana upendo na ni mzuri sana, wivu ndiyo ulipelekea sisi kuvurugika, sasa hivi huwa tunawasiliana mara moja moja ila namkubali”.