Klabu ya Liverpool imewakodia ndege wachezaji wake wawili, Sadio Mane na Mohamed Salah ambao wanakwenda kushiriki utoaji wa tuzo za Mchezaji Bora wa Afrika nchini Ghana.

Wachezaji hao wanatarajiwa kuondoka kwenye klabu hiyo kesho kutwa Alhamisi na kutarajiwa kurejea usiku huohuo nchini England.

Liverpool wametoa taarifa kuwa wachezaji hao watakodiwa ndege na ilikwenda nchini Ghana kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za utoaji wa tuzo hizo ambazo wote wawili wanashiriki.

Kwa upande wa kocha wa timu hiyo, Jurgen Klopp amesema kuwa anaamini wachezaji hao wanaweza kwenda na kurejea England kucheza mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Everton siku ya Ijumaa.

Salah bado anasumbuliwa na majeraha ya nyonga ambayo yalimfanya aukose mchezo wa juzi dhidi ya Burnley na kocha huyo amesema kuwa kama atakuwa hawajapona hadi Ijumaa basi hatacheza mchezo dhidi ya Everton.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *