Klabu ya soka ya Liverpool ya Uingereza imekamilisha usajili wa beki kutoka Southampton, Virgil van Dijk kwa kitita cha paundi milioni 75.

Beki huyo wa timu ya taifa ya Uholanzi amefanyiwa vipimo vya afya jana na ametajwa kuwa atakuwa analipwa kiasi cha paundi 200,000 kwa wiki.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mtandao wa Liverpool umesema kuwa mchezaji huyo atahamia rasmi katika timu hiyo Jumatatu ya January 1, 2018 dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa.

Mpaka sasa Liverpool imeshasajili wachezaji sita kutokea Southampton akiwemo Rickie Lambert (£5m), Adam Lallana (£28m), Dejan Lovren (£23m), Nathaniel Clyne (£16m), Sadio Mane (£37m) na Virgil van Dijk (£75m) ambapo wametumia jumla ya paundi milioni 184 kusajiliwachezaji wote hao.

Kutokana na usajili huo Dijk anakuwa mchezaji wa pili ndani ya Uingereza kusajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha baada ya Paul Pogba aliyesajiliwa na Manchester United katika msimu uliopita kutokea Juventus kwa kiasi cha paundi milioni 89.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *